Watu wasiojulikana wamekata nguzo tano na kuiba taa za barabarani zinazotumia umeme wa jua zinazotajwa kuwa na gharama kubwa zaidi ya shilingi milioni 20 kisha kutelekeza gari aina ya Toyota Hiace walilokuwa wakilitumia kufanya uhalifu huo katika barabara mpya ya bigwa nanenane manispaa ya Morogoro.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Kamishna msaidizi wa polisi Wilbroad Mutafungwa amesema kufuatia tukio hilo hadi kufikia sasa watuhumiwa sita wamekamatwa pamoja na gari walilokuwa wakitumia huku msako mkali ukiendelea wa kuwasaka watuhumiwa wengine.