Back to top

Watumishi wa umma kesho wanaanza kutumia mfuko mpya wa PSSF.

31 July 2018
Share

Serikali kuanzia kesho inaanza kutumia sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa umma namba 2 ya mwaka 2018 ambayo imeunganisha mifuko minne ya hifadhi ya jamii na kuunda mfuko mmoja wa PSSF.

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge kazi,vijana ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama amesema sheria hiyo imeunganisha mifuko ya LAPF,GPEF,PPF NA PSPF na kufanya marekebisho ya shirika la Taifa la hifadhi ya jamii NSSF kuufanya mfuko utakaohudumia wafanyakazi wa sekta binafsi na sekta isiyo rasmii.

Aidha kuhusu mikataba na rasilimali na madeni yaliyokuwa katika mifuko iliyounganishwa itaamishiwa katika mifuko iliyounganishwa pamoja na watumishi wa mifuko hiyo wataamishiwa katika mfuko mpya wa PSSF ambapo uongozi wa mfuko utawapangia majukumu yao kwa kuzingatia muundo wa mfuko huo .

Aidha akijibu swali waandishi wa habari Mhe Jenista amesema kwa mujibu wa sheria hiyo sasa mifuko hiyo itakuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu badala ya  mamlaka ya udhibiti wa mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo kwa mujibu wa sheria iliyounda SSRA itaendelea kuwa mdhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii.

Mkuu wa PSSF Bwana Eliud Sanga ameahidi kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa ikiwemo kuondoa kero ambazo wanachama wa mifuko hiyo wamekuwa wakipata kwa muda mrefu.