
Afisa Mfawidhi Bodi ya Nyama Kanda ya Kaskazini, Bw.Patrick Kaaya, amewataka Wafanyabiashara wa nyama nchini kutumia zana za kisasa ili kulinda afya ya mlaji.
Bw.Patrick ameeleza hayo Jijini Arusha na Kubainisha kuwa bodi hiyo imekuwa ikiwachukulia hatua watu wanaokiuka sheria na taratibu na miongozo ya bodi hiyo, ili kuweka mazingira bora ya walaji Wanyama ambapo amewataka wafanyabiashara hao kufuata taratibu zilizopo.


Amesema Bodi ya Nyama Kanda ya Kaskazini, imetoa elimu na kuonyesha vifaa sahihi ambavyo vinatakiwa kutumika kwenye maduka ya nyama, na kwamba mbali na kutoa elimu hiyo Bodi imekuwa ikichukua hatua za kisheria kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaokiuka sheria.
