
Wakala wa Vipimo mkoa wa Mtwara umetoa miezi miwili kwa wafanyabiashara wanaouza gesi inayotumika majumbani kuhakikisha wanakuwa na mizani ya kupima bidhaa hiyo ili kuhakikisha mteja hapunjiki.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Wakala wa vipimo mkoa wa Mtwara, Sadi Haruna, wakati akitoa elimu kwa wafanyabishara wa gesi ya kupikia majumbani kutambua sheria ya ya vipimo ili kuondokana na makosa ambayo yanaweza kusababisha kutozwa faini.
Amesema uwepo wa mizani utamwezesha mteja, kutambua uzito wa gesi iliyopo kwenye mtungi, ambapo uzito huo unatakiwa kuandikwa juu ya mtungi ili kumwenzesha mteja kutambua hilo.
Amesema pia mteja anatakiwa kutambua uzito wa mtungi ukiwa hauna gesi lakini pia uzito wa gesi yenyewe inayotoka katika mtungu huo lengo likiwa mteja kupata bidhaa bora na inayokidhi viwango.
Mizani hizo zitatakiwa kuhakikiwa na wakala wa vipimo na si vinginevyo.