Back to top

Wavuvi Watanzania wajifanya askari wa Uganda, wapora, wafanya mauaji.

04 February 2020
Share

Umoja wa wavuvi wa samaki mkoa wa Mwanza na Mara wamesema kumeibuka matukio ya baadhi ya wavuvi Watanzania ambao wanatumia sare za askari wa nchi jirani ya Uganda na kujifanya maofisa wa polisi wa nchi hiyo ambapo huwavamia wenzao kwa kutumia silaha na kufanya matukio ya mauaji, kuiba samaki na zana za uvuvi.

Hayo yameelezwa wakati wa kikao cha wadau wa uvuvi na kamati za ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza na Mara kilichofanyika mkoani humo kikiusisha wavuvi kutoka wilaya tano za mikoa hiyo.

Rajabu Ndonyi ni mvuvi akisimulia kadhia wanayokumbana nayo, kwa baadhi ya wavuvi wa Tanzania kutumia kivuli cha askari wa Uganda, Kupora, kufanya mauaji ya wavuvi ziwa Victoria nk.

Inaelezwa katika siku za karibuni kumekuwa na matukio ya wizi na utoroshaji wa samaki kwa njia za magendo na mauaji ya wavuvi ziwani  na kudai kuwa wanaofanya hayo ni wavuvi wenyewe kwa kutumia kivuli cha askari wa Uganda.

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Ukerewe na Mkuu wa wilaya ya Musoma wamesema kuwa watahakikisha wanashirikiana na wavuvi kukomesha matukio ya wizi na uvuvi haramu.