Watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi huko wilayani Korogwe mkoani Tanga kutokana na kusababisha uvunjifu wa amani wanaouleta katika kijiji cha Kwema zandu huko Korogwe Tanga.
Kabla Jeshi hilo halijawakamata watu hao kufuatia amri ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani hapo baadhi ya wanannchi wa kijiji hiki walianza kuwalalamikia watu hawa huku baadhi yao wakidai kuwa mmoja wa watu hao hafahamiki alikotoka na hali hiyo imewafanya wananchi kutokuwa na imani na watu hao.
Kufuatia malalamiko haya mkuu wa wilaya akamwamuru mkuu wa polisi kuwakamata watu hawa kwa mahojiano zaidi.
Baada ya hapo akatoa wito kwa wananchi wote wilayani hapa kutoa taarifa serikali kwa watu wanao weza kusababisha uvunjifu wa amani hasa kipindi hiki hali iliamsha shangwe ya furaha kwa wananchi hawa.