Back to top

WAZIRI MABULA ATETA NA MKURUGENZI WA TAASISI YA RRI

29 August 2023
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo yavMakazi Mhe. Dkt Angeline Mabula, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasiliamali kutoka Marekani Bw. Patrick Kipalu.

Dkt.Mabula amekutana na mkurugenzi huyo anayeshughulika na Programu za Haki na jitihada za Rasilimali Ardhi katika Bara la Afrika katika ofisi ya Wizara eneo la Mtumba Jijini Dodoma.

Mazungumzo ya viongozi hao mbali na mambo mengine yamelenga maandalizi ya Kongamano la Nne la Kimataifa litakalofanyika jijini Arusha kuanzia 12- 15 Septemba 2023 likiwa na  agenda kuu ya upatikanaji wa hatimilki za ardhi.

Taasisi hiyo ya Marekani ndiyo wadhamaini wa kongamano hilo linalojadili masuala mbalimbali yahusuyo masuala ya ardhi ikiwemo hati milki za ardhi.