Back to top

Waziri Mhe.Jaffo achukizwa na udhalilishaji wa kingono kwa watumishi

09 December 2018
Share

Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe.Suleiman Jaffo amemtaka mkuu wa mkoa wa Katavi kuunda timu ya uchunguzi dhidi ya tuhuma za udhalilishaji wa kingono vinavyofanywa na baadhi ya wakuu wa idara dhidi ya watumishi wa kike wa halmashauri ya Mlele
 
Mheshimiwa Jaffo ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi na wananchi alipofanya ziara mkoani Katavi,na kusema tayari amekwishapokea malalamiko kadhaa kuhusiana na vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya kazi
 
Pia amemtaka mkuu huyo wa mkoa kuchunguza tuhuma za uuzwaji wa magari ya serikali bila kufuata utaratibu pamoja na ubadhirifu wa fedha katika ujenzi wa shule ya sekondari inayojengwa na shule ya msingi Kusa zilizopo wilayani humo

 
Awali akitoa taarifa kwa waziri huyo mkuu wa mkoa wa katavi Amos Makala amesema mkoa umejipanga katika kusimamia masuala ya kipaumbele kama elimu na afya