Back to top

Waziri Mkuu atoa wiki mbili akute madawati Mwarusembe –Mkuranga.

13 August 2020
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wiki mbili kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa wilaya ya Mkuranga na Mkurugenzi Mtendaji wake wahakikishe shule za msingi na sekondari za Mwarusembe zinakuwa na madawati.

Ametoa agizo hilo Agosti 13, 2020 wakati akizungumza na wananfunzi na walimu wa shule ya msingi Mwarusembe alipofanya ziara ya kushtukiza katika shule hiyo na kukuta baadhi ya wanafunzi wamekaa chini.

Waziri Mkuu alisema mkoa huo unaongoza kwa idadi kubwa ya viwanda, na wilaya hiyo peke yake ina viwanda 75 lakini haijaweza mbinu za kupata madawati. “Halmashauri yenu ina viwanda vingi kuliko wilaya zote, hivi vyote vinafanya nini? Kwa nini msiende kwenye viwanda vyenu mkaongee nao ili fedha ya CSR itumike kuondoa tatizo hili? Mapato yenu kwa mwaka ni zaidi ya shilingi bilioni mbili, zinafanya nini?”

Waziri Mkuu amesema ukosefu wa madawati unawafanya walimu washindwe kusimamia usafi kwa wanafunzi lakini pia unawapa mzigo wazazi wa kununua sabuni ili watoto wao wafue nguo kila siku.

 "Nataka Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri na wakuu wa idara hasa wa elimu mjipange upya katika suala la madawati. Nikija tena na nisipokuta madawati, mjiandae..."