Back to top

Waziri wa Usalama aliyetangaza kugombea Urais Uganda akamatwa.

12 March 2020
Share

Maafisa wa usalama kitengo maalum cha ujasusi,CMI wamemkamata aliyekuwa Waziri wa usalama nchini Uganda Jenerali Henry Tumukunde, wiki moja baada ya kuwasilisha ombi la kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Tumukunde amekamatwa akiwa katika ofizi zake eneo la Kololo jijini Kampala, haijabainika ni wapi alikopelekwa.

Tumukunde aliyekamatwa amewahi kuhudumu kama mkuu wa idara ya ujasusu nchini Uganda.