Back to top

WHO yasema maambukizi ya Corona yanaongezeka ulimwenguni.

01 August 2021
Share

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) DKT.Tedros Adhanom, amesema matukio ya maambukizi ya virusi vya Corona yanaongezeka tena ulimwenguni na ongezeko hili linatokana na virusi aina ya Delta.

Dkt.Tedros amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya shirika hilo Mjini Geneva kupitia njia ya video.

Amesema kwamba karibu maambukizi milioni 4 mapya ya Corona yaliripotiwa kwa shirika hilo wiki iliyopita na kwamba wanatarajia maambukizi kuzidi Milioni 200 ndani ya wiki mbili.

Kwa wastani, maambukizi katika maeneo matano kati ya sita ya Shirikala Afya Duniani  yameongezeka kwa asilimia 80, au karibu mara mbili, katika wiki nne zilizopita.

Barani Afrika, vifo vimeongezeka kwa asilimia 80 katika kipindi hicho hicho.