Back to top

WIZARA YAWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA KAMATI

13 March 2023
Share

Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo na kuwasilisha taarifa ya muundo na majukumu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, taarifa ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa Bwawa la kuvuna maji kwa ajili ya kunyweshea mifugo la Matekwe lililopo Nachingwea, Mkoani Lindi, na taarifa ya ujenzi wa bandari ya uvuvi iliyopo Wilayani Kilwa, Mkoani Lindi.

Baada ya kupokea taarifa hiyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. David Kihenzile  alimuhakikishia Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega  kuwa watashirikiana bega kwa bega na Wizara ili kuiwezesha kufikia malengo yake ya kuwahudumia wananchi ili wapate maendeleo  katika shughuli zao za kila siku za ufugaji na uvuvi.

Aidha, kamati hiyo inatarajiwa kufanya ziara Mkoani Lindi hivi karibuni kwa ajili ya kutembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo.