
Idara ya Haki nchini Marekani kwa kushirikiana na wanasheria wengine 16 wa Serikali, wamefungua kesi, wakiishutumu kampuni ya Apple inayojishughulisha na utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki zikiwemo Simu Janja za iPhone, kwa kuwawekea vikwazo washindani wake kinyume cha sheria ili kuhodhi soko la simu na ushindani kwenye bidhaa hizo.
.
Malalamiko hayo yanaishutumu Apple kwa kukandamiza uvumbuzi na ukuaji wa programu mpya na kupunguza mvuto wa bidhaa pinzani hali ambayo imeelezwa kuwa inasababisha watumiaji wa iPhone kuwa tegemezi kwa Apple na bidhaa zake pekee.
.
Hata hivyo kampuni ya Apple imekana madai hayo, ambapo imebainisha kuwa endapo kesi hiyo itafanikiwa itaathiri uwezo wao wa kuunda teknolojia ambayo watu wanatazamia kuipata kutoka kwenye kampuni hiyo.
