
Serikali imesema imepokea hoja ya kubadilisha kikokotoo na kwamba inaifanyia uchambuzi zaidi.
.
Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Philip Mpango, alipomuwakilisha, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), ambayo Kitaifa imefanyika Jijini Arusha, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
.
"Serikali imepokea hoja kuhusu kubadilisha kikokotoo kwa ajili ya kuifanyia uchambuzi zaidi maana kama ilivyosemwa kwenye risala wafanyakazi hawaridhishwi na kanuni hizo na Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na Serikali yake ni wasikivu sana" Ameeleza Mhe. Dkt.Mpango.