
Watumishi wa Umma wamehimizwa kujitokeza kuchunguza afya zao, katika Kambi ya Matibabu na Uchunguzi inayofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba.
Wito huo umetolewa na Ndg.Cyrus Kapinga, ambae amemuwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo.


Ndg. Cyrus amesema huduma hizo zinatolewa bure kwa watumishi wote watakaofika kupata huduma.
"Huduma katika kambi hii ni bure kabisa kwa wale wote watakaofika kupata huduma na kwa watakaobainika kuwa na changamoto watapata rufaa ya kwenda kuendelea na uchunguzi wa kina pamoja na matibabu katika Hospital ya Kanda Benjamin Mkapa," amesema Ndg.Cyrus
Kwa upande wake, Prof.Abel Makubi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, ameshukuru Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kutoa eneo la kufanyia kambi hii ya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali na kushirikiana katika kufanikisha kuwepo kwa kambi hii.

Bi.Sophia Kayombo, ambaye ni mtumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ameshukuru BMH kwa huduma nzuri alizopatiwa na madaktari wa BMH.
Kambi hii ambayo imeanza Agosti 5, 2024 na inafikia tamati Agosti 9, 2024.
