Back to top

BASHUNGWA:TUKITAKA KUPATA VIONGOZI WAZURI, TUKAJIANDIKISHE 

09 August 2024
Share

Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa, ametoa wito kwa Watanzania wenye sifa za kujiandikisha katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura, kujitokeza katika vituo, ili kupata Kitambulisho cha mpiga kura kitakachowawezesha kupata haki ya kuchagua Viongozi katika Chaguzi zijazo.

Bashungwa ametoa wito huo mara baada ya kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, katika Kituo cha Shule ya Msingi ya Ahakishaka, Kata ya Nyabiyonza Wilayani Karagwe Mkoani Kagera.

"Tukitaka kupata viongozi wazuri hatua ya kwanza ya kufanya ni kujiandikisha kwenye daftari ili tuweze kutumia haki yetu ya kidemokrasia muda utakapofika wa uchaguzi"Amesema Bashungwa.

Bashungwa ameipongeza Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, kwa kuboresha zoezi hilo na kufanya kazi kwa weledi inayoimarisha demokrasia nchini.