Back to top

MKAKATI WA UTALII DODOMA KUONGEZA UKUSANYAJI KODI NCHINI

22 August 2025
Share

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa uzinduzi wa mkakati wa Utalii Mkoani Dodoma utasaidia kuongeza wigo wa mapato ya serikali kupitia ukusanyaji wa kodi mbalimbali.

Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Dodoma, Bw. Pendolake Elinisafi katika uzinduzi wa Mkakati wa Utalii Mkoani hapa ambapo Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Waziri wa Viwanda na Biasha, Mhe. Dkt. Selemani Jafo.

Bw. Elinisafi amesema kuwa mkakati huo sio tu unasaidia kuinua pato la taifa, bali pia unaimarisha misingi ya mapato ya ndani kupitia kodi.

Aidha  amesema kuwa mkakati huo utaongeza  wigo wa walipa kodi, kwa kukuza utalii, biashara nyingi mpya zitachipuka kama hoteli, migahawa, wasafirishaji wa watalii, watoa huduma za burudani na maduka ya bidhaa za utalii wote hao wanakuwa walipakodi wapya.