Back to top

TADB YANG'ARA TUZO ZA UBORA WA TAARIFA ZA FEDHA

26 November 2026
Share

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imechaguliwa kuwa miongoni mwa washindi wa Tuzo za Ubora wa Uandaaji na Uwasilishaji wa Taarifa za Fedha kwa mwaka 2025 (Best Presented Financial Statements Awards), zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo imefanyika leo, Novemba 26, 2026, katika Ukumbi wa APC, Bunju, jijini Dar es Salaam.

Mafanikio hayo yanaonesha dhamira ya TADB katika kuzingatia viwango vya kimataifa vya uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za fedha, huku ikiimarisha uwazi, uwajibikaji na utawala bora pamoja na kutekeleza matakwa ya kisheria na kiudhibiti.

Tuzo hiyo inaendelea kuimarisha hadhi ya TADB kama taasisi ya fedha ya maendeleo inayozingatia weledi, uwazi na ubora katika utekelezaji wa majukumu yake.