Wakulima wa zao la Korosho katika halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani lindi, wameshauriwa kusafisha mashamba yao ya Mikorosho ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo la biashara kama ilivyokuwa msimu wa mwaka 2017/2018.
Ushauri huo umetolewa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2018, Charles Kabeho, wakati alipotembelea shamba darasa la Mikorosho la mkulima wa zao la Korosho Hassani Chikawe, katika kijiji cha Legezamwendo.
Kwa upande wake mkulima wa shamba hilo, Hassani Chikawe licha ya kupata fedha nyingi kwa ajili ya mauzo ya Korosho lakini amelalamikia wanyama waharibufu aina ya Tembo.