Serikali imelitengua katazo la wananchi kuzuiwa kupanda meli hadi wawe na vitambulisho jijini Mwanza.
Katazo hilo limekuja ikiwa ni siku tatu mfululizo kufuatia vurugu zilizoibuka jijini Mwanza za wananchi kuzuiwa kupanda meli za serikali hadi wawe na vitambulisho.
Akizungumza na ITV mkoani Njombe Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Mheshimiwa ATASHASTA NDITIYE amesema suala hilo siyo sahihi na ni uhujumu uchumi.
Mheshimiwa NDITIYE amewataka wananchi waachwe waendelee na safari zao hadi pale serikali itakapokaan kujadili kiini cha tatizo hilo.
Aidha, amewaomba radhi wananchi wa jiji la Mwanza kutokana na usumbufu walioupata.