Back to top

Wakulima wa michikichi walalamikia teknolojia duni ya ukamuaji.  

18 October 2018
Share

Wakulima na wachakataji wa zao la chikichi katika kijiji cha Ilagala wilayani Uvinza mkoani Kigoma wamelalamikia teknolojia duni wanayoitumia kukamua mafuta ya mawese ambayo  imekuwa ikishindwa kuwasaidia kupata mafuta bora na ya kutosha hali inayosababisha kukosa soko la uhakika ndani na nje ya nchi na kuiomba serikali kuwasaidia kupata teknolojia mbadala na mikopo yenye riba ndogo.

Meneja wa kituo cha teknolojia kutoka Shirika la viwanda vidogo nchini SIDO mkoani Kigoma Mabamba Majogoro amesema shirika hilo limekuja na teknolojia mpya itakayosaidia kuondoa changamoto hizo huku akitoa wito kwa wakulima hao kuwa tayari kutumia teknolojia ambayo itawasaidia kunufaika na zao la chikichi.