Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amepiga marufuku uchomaji matofali kwa kutumia kuni katika maeneo ya mijini na badala yake kushauri matumizi ya pumba kufanyia akzi hiyo.
Mh. Kanyasu alipozungumza na kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Geita.
Amesema uchomaji matofali kwa kutumia nishati ya kuni umekuwa ukichangia upotevu mkubwa wa misitu hali inayotishia sehemu kubwa ya nchi kuwa jangwa.