Back to top

Mbunge wa Kawe Mh.Halima Mdee ahojiwa na kamati ya bunge kwa saa 2

22 January 2019
Share

Mbunge wa jimbo la Kawe kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh.Halima Mdee, ameitikia wito wa Spika Job Ndugai wa kwenda kuhojiwa katika kamati ya kudumu ya bunge ya haki, maadili na madaraka ya bunge kutokana na kuunga mkono maneno ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) Prof.Mussa Assad kuwa bunge nidhaifu.
 
Mh.Mdee akiwa ameongozana na mbunge wa Bunda Mh.Esther Bulaya amewasili katika viwanja vya bunge jijini Dodoma majira ya saa tano kamili asubuhi na kupandisha ngazi ghorofa ya kwanza ulipo ukumbi wa mheshimiwa spika.
 
Hata hivyo mahojiano hayo yaliyomalizika saa saba na dakika ishirini na nane mchana yalihitimishwa na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya haki, maadili na madaraka ya bunge, Mh.Emmanuel Mwakasaka, ambaye amesema taarifa itafikishwa kwa spika kwa ajili ya kutolea maamuzi.
 
Mhe.Halima Mdee amehojiwa leo januari shirini na mbili ambapo januari ishirini na moja alihojiwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) Prof.Mussa Assad kwa zaidi ya saa tatu mbele ya kamati ya kudumu ya bunge haki maadili na madaraka ya bunge.