
Watu wawili ambao ni raia wa Afrika Kusini wamefariki baada ya ndege waliokuwa wakiitumia kusafiria kutoka nchini Uganda kuanguka wilayani Sikonge mkoani Tabora na kuteketea moto.
Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Sikonge Peres Magili amesema kwamba Ndege hiyo ilikuwa inatokea Uganda wanja wa Entebbe, dege hiyo mali ya kampuni ya U-Dream Global Oparetor ndipo ikatua eneo hilo kwa dharura baada ya kuchemka, hivyo leo asubuhi nanusu iliondoka uwanja wa ndege wa Tabora baada ya muda kidogo ilivyoondoka ndege hiyo ikaleta tena matatizo ndipo wakawasiliana na wahusika wa uwanja wa ndege wakashauriana warudi, wakati wakiwa njiani kurudi ndipo ndege yao ikadondoka na kuteketea moto.
Mkuu huyo wa wilaya Magili amesema Ndege hiyo ilikuwa inaelekea Lilongwe Malawi na baada ya kupata hitilafu ndipo ikatua jambo ambalo mamlaka ya uwanja wa ndege ilikuwa haina taarifa juu ya ndege hiyo, kufuatia tukio hilo sasa mkuu huyo wa wilaya amesema wamekusanya majivu na kuyapeleka hospitali ya Tabora kwa ajili ya uchunguzi.
Video hii hapa chini inamaelezo ya kina fuatilia hapo