Wananchi wa kijiji cha Nditi halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi wameiomba serikali kuwapa idhini ya kuendelea kuchimba madini yaliyopo katika mgodi wa Nditi wilayani humo, baada ya serikali kuwafutia leseni ya uchimbaji wawekezaji waliokuwa wakichimba madini katika mgodi huo.
Wananchi hao wametoa kilio hicho mbele ya waziri wa madini, Mhe.Dotto Biteko alipopafanya ziara ya siku moja katika wilaya hiyo ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea mgodi huo wa Nditi na kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho
Kufuatia kilio hicho cha wananchi wa kijiji cha nditi,
wilayani nachingwea, mkoani lindi,waziri Biteko, amewaomba wananchi hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambapo suala lao likishughulikiwa kwa mujibu wa sheria.