Back to top

Vijiji 76 kuwa na umeme wa uhakika 2021 mkoani Lindi.

25 February 2020
Share


Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu, amesema hadi kufikia mwezi juni mwaka 2021 vijiji vyote 76 vya wilaya ya Liwale, mkoani Lindi vitakuwa vimeshaunganishiwa huduma ya umeme.

Mhe.Mgalu ametoa kauli hiyo mara baada ya kuwasha umeme katika shule ya msingi Naluleo pamoja na zahanati ya Makata kisha kuzunguza na wananchi huku akiwahakikishia wananchi hao kuwa hakuna kijiji kitakachoachwa bila kuunganishiwa umeme wala nyumba ambayo itarukwa, nyumba zote zinawekewa huduma hiyo umeme iwe nyumba ya bati ama nyumba ya fulusuti.

Amesema hadi sasa vijiji vilivyounganishiwa umeme kwa wilaya ya Liwale ni vijiji 36 na vilivyobaki ni vijiji 40 tu na hadi kufikia juni mwaka 2020 vijiji vyote vitafikiwa.

Hata hivyo Mhe.Mgalu amewataka wananchi wa vijiji hivyo kutumia umeme huo kwa faida kwa kufanya shughuli za maendeleo kwa kuanzisha shughuli za kuchomelea, kuranda mbao pamoja na kuanzisha mashine za kusaga nafaka.

Wakizungumza na ITV baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mpengere wilaya ya Liwale, ameishukuru Serikali kwa kuwapelekea umeme kijijini kwao kwani umeme huo sasa utawasaidia kufanya shughuli za maendeleo na kujiingizia kipato zaidi.