Siku chache baada ya ITV kuripoti zahanati ya kijjiji cha Kajima kata ya Jakika wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kuwa na mtumishi mmoja ambaye akiwa na dharura inafungwa na wananchi wanakosa huduma za matibabu serikali imeongeza mtumishi mmoja kwenye zahanati hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Bw. Gaspar Balyomi amesema kuwa hategemei kuona wananchi wakikosa huduma za matibabu katika kijiji hicho kwa zahanati kufungwa kwa kuwa kwa sasa watakuwa wakipokezana pindi mmoja anapokuwa na dharura.