Back to top

JPM ampigia simu kumpa pole Zitto Kabwe baada ya ajali Kigoma.

07 October 2020
Share

Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli amempigia simu na kumpa pole Mhe.Zitto Zuberi Kabwe aliyepata ajali ya gari jana Mkoani Kigoma.  

Amemuombea heri ili apone haraka na pia amewashukuru Madaktari na Wauguzi wa Kituo cha Afya cha Kalya na Hospitali ya Maweni kwa matibabu waliyompa.