Back to top

“Suala la kilimo sio suala la wizara ya kilimo peke yake”.Bashe

14 April 2021
Share

Wizara ya kilimo imewaagiza wakurugenzi wote wa Halmashauri nchini kitenga fedha kwenye ofisi zao kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji ambacho kwa sasa kimeendelea kupata tija na kimsaidia mkulima kujipatia kipato.

“Suala la umwagiliaji na suala la kilimo sio suala la wizara ya kilimo peke yake, ni suala ambalo linatuhusu pamoja, tuwaombe wakurugenzi wa halmashauri kwa kuwa moja ya chanzo cha mapato wanachokipata kinatokana na mazao ni lazima asilimia 20 ambayo imeelekezwa na Mhe.Waziri Mkuu..wairudishe katika sekta ya kilimo”.Bashe

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe ametoa agizo hilo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Dokta Oscar Kikoyo Mbunge wa Muleba Kusini aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuendeleza skimu za umwagiliaji ambayo imetelekezwa kwa sasa.

“Nikiri mbele waheshimiwa wabunge na  watanzania wote kwamba hatuwezi kutoka katika matatizo ya kilimo bila kuwekeza katika umwagiliaji na huo ndio muelekeo wa serikali na maelekezo ya ilani ya CCM”.Naibu waziri Kilimo Hussein Bashe.

Mh Bashe amesema mipango ya serikali kwa sasa kukamilisha miradi yote ya umwagiliaji iliyoanzishwa na Wizara haina mpango wa kuanzisha miradi mipya kwa kuwa iliyopo kwa sasa imeendelea kuwa na tija kwa wakulima.

Pamoja na mipango hiyo Mh bashe amesema serikali imetenga fedha za kutosha kwenye tume ya umwagiliaji kwa lengo la kubadili mfumo wake wa ufanyaji kazi na kuipatia vifaa vipya vya kisasa kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji kote nchini.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi Mh Abdallah Ulega amesema wizara yake imepanga kuboresha na kujenga upya mnada wa Pugu Dar es salaam kwa kuwa umechangia kukuza pato la.taifa.