Back to top

Wananchi Madaba walalamikia kupigwa, kunyanyaswa na kuporwa Mali zao.

25 April 2021
Share

Wananchi wa Kijiji cha Mbangamawe katika Halmashauri Wilaya ya Madaba Mkoani Ruvuma wamelalamikia kupigwa, kunyanyaswa, kuporwa Mali zao na kuchomewa vibanda vyao vya kuishi na Askari wa Maliasili wakidaiwa kuishi na kufanya shughuli zao kwenye Mapitio ya Wanyamapori.
 
Akizungumzia tukio hilo Waziri wa Maliasili na Utalii Dokt Damas Ndumbaro amesema Serikali haitakubali Wananchi wanyanyaswe hivyo itaunda Tume kuchunguza tukio hilo.