Back to top

Kuongezeka kwa wagonjwa wa mafua ni hali ya kawaida.

18 December 2021
Share

Kufuatia kuenea kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha kuwa watu wengi wana dalili za kukohoa, mafua, maumivu ya mwili na kuchoka, Wizara ya Afya imefuatilia na kugundua kweli kuna ongezeko la wananchi kupata dalili hizo ambapo imebainisha kuwa hali hiyo ni ya kawaida kila mwaka(seasonal influenza) ambayo huchangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
.
Hata hivyo Wizara hiyo imewashauri wananchi wanapopata dalili hizo watoe taarifa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa uchunguzi wa kitaalamu ili wapatiwe matibau stahiki.