Back to top

LEO NI SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE.

11 October 2022
Share

Tarehe 11 Oktoba ya kila mwaka, Tanzania inaungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa, kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, ambapo lengo ni kutoa fursa kwa wadau wanaotekeleza afua za watoto, hususani watoto wa kike, kufanya tathmini ya upatikanaji wa haki, ulinzi na maendeleo ya watoto kwa ujumla, na kupendekeza hatua stahiki katika kuboresha huduma hizo.

Kwa Mwaka huu 2022, Kauli mbiu inayoongoza Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, ni “Haki Zetu ni Hatima Yetu; Wakati ni Sasa”.