
Uingereza imesema itawaondoa wanajeshi wake 300, kwenye jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa MINUSMA nchini Mali, kufuatia hatua za nchi nyingine za Magharibi kuchukua hatua hiyo.
Waziri wa Ulinzi James Heappey, amewaambia wabunge kuwa, wanajeshi wa Uingereza wanaondoka kwa sababu kuendelea kwa mapinduzi ya kijeshi nchini Mali, kunazuia jitihada za Jumuiya ya Kimataifa kuleta utulivu nchini humo.
Hatua hii ya Uingereza imekuja baada ya Ufaransa kuamua kuwaondoa maelfu ya wanajeshi wake nchini Mali, kufuatia uongozi wa kijeshi katika taifa hilo la Afrika Magharibi, kuanza kushirikiana na kundi la kibinafsi la usalama la Wagner kutoka nchini Urusi.
