Back to top

MABULA ASIKITISHWA WANANCHI KUTOCHANGAMKIA HATI .

21 December 2022
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula, ameonesha kutoridhishwa na kasi ya wananchi wa wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam ,kutochangamkia fursa ya kupatiwa hati kupitia zoezi la urasimishaji makazi holela.

Hali hiyo imejitokeza wakati wa utoaji hatimiliki za ardhi kwa wananchi 1081 wa maeneo tofauti wilayani Ubungo, waliokamilisha taratibu za kumilikishwa ardhi kupitia zoezi la urasimishaji makazi holela, eneo la Stop Over kata ya Saranga Dar es Salaam.

Amesema urasimishaji katika wilaya ya Ubungo, Dkt Mabula alisema kazi kubwa imefanywa na ofisi ya ardhi halmashauri ya Ubungo ambapo hatimiliki 1081 zimekamilishwa na kugawiwa kati ya viwanja 23,967 vilivyopimwa na kuidhimishwa.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, changamoto ya zoezi  urasimishaji  makazi holela ipo pande zote mbili za wananchi na makampuni yanayofanya kazi za urasimishaji ,na kusema kuwa haiwezekani hati 1081 pekee, ndiyo zikamilishwe na kugawiwa wananchi kati ya viwanja 23,967 vilivyoidhinishwa.