
Waziri wa TAMISEMI Mhe.Angellah Kairuki amekerwa na hali ya 55.2% ya wanafunzi waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mkoani Tanga kutoripoti shule ambapo amebainisha kuwa asilimia kubwa imechangiwa na Wilaya ya Kilindi ambayo ni 11% pekee ndio wameripoti shule huku Korogwe Mji ikiwa ni 22.78%, Korogwe TC 30.21%, Handeni TC 42.55%, Handeni DC 45.86%, Bumbuli 53.26%, Mkinga 27.98%, Muheza 50%, Pangani 52 na Tanga jiji 76.23.
.
Mhe. Kairuki ametoa kauli hiyo mkoani Tanga, wakati akizungumza na Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule za Sekondari, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na viongozi wa Elimu ngazi ya Halmashauri kwenye kikao kazi cha Uboreshaji wa Usimamizi wa Elimumsingi na Sekondari katika shule ya sekondari Tanga ufundi.
