
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha mgogoro wa kupanda gharama za maisha nchini Uingereza unaweza kuzidisha kiwango cha wanawake wanaokufa wakati na baada ya ujauzito.
Ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani imeonya hali hiyo inashuhudiwa, huku ukosefu wa usawa wa kiafya ukizidi kuwa mbaya zaidi kwa akina mama wajawazito wanatumbukia katika umaskini.
Aidha Ripoti hiyo imeeleza kuwa, asilimia 9.6 ya akina mama wajawazito nchini Uingereza katika kila watoto laki moja wanaozaliwa, hufariki dunia wiki sita tu baada ya kujifungua.
Dkt.Natasha Azzopardi mmoja wa maafisa wa WHO na Daktari aliyebobea katika afya ya uzazi nchinii Uingereza amesema kuna uhusiano unaoonekana kati ya uwezekano wa mwanamke kufa katika wiki za awali kabla na baada ya kujifungua kutokana na uwepo wa kiwango cha juu cha umasikini.
Ameongeza kusema kuwa, Shirika la Afya Duniani (WHO) lina wasiwasi na hali ya wanawake nchini Uingereza hasa kutokana na kupanda kwa gharama za maisha na hali hiyo inaweza kuwa mbaya zaidi katika siku za usoni.
