Back to top

UJENZI JENGO LA KINAMAMA CHONGOLO ATOA MAAGIZO

29 January 2023
Share

Wananchi wa Kijiji cha Wami Dakawa, wilayani Mvomero mkoani Morogoro, wamemuomba Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, kufuatilia ukamilishwaji wa jengo la kinamana kwenye Zahanati ya Kijiji hicho, kutokana na sasa kulazimika kujifungua bila usiri, huku jengo kwa ajili ya kina mama kujengwa muda mrefu bila kukamilishwa.

Kutokana na malalamiko hayo  Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mvomero Dkt Phillipina Titus, na Mwenyekiti wa Halmashauri, hiyo kubadili matumizi ya fedha za miradi mingine, Ili kumalizia jengo hilo na kutoa shilingi milioni moja za kuanzia kazi hiyo.

.