
Baadhi ya wafugaji jamii ya kimasai katika Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro ,wameanza kufuga kisasa na kuachana na tabia ya kufuga mifugo mingi ambayo imekuwa haina tija kwao, huku wakati mwingine ikisababisha kuwepo kwa migogoro baina yao na wakulima hasa katika kipindi cha kiangazi wakati wa kutafuta malisho.
