
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi kwa ujumla kuendelea kuiamini Serikali yao kwa sababu watendaji wake wamejipanga kuwatumikia kwa weledi, uadilifu na uaminifu wa hali ya juu.
.
Mhe.Majaliwa ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Miaka 46 ya Chama hicho, ambayo kitaifa yamefanyika wilayani Biharamulo, mkoani Kagera, ambapo amebainisha kuwa Mhe.Samia Suluhu Hassan amefanya maboresho makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo ya uwekezaji, lengo likiwa ni kukuza uchumi wa Taifa na wa mwananchi mmoja mmoja.
