Back to top

NBS: IDADI YA WATALII ILIONGEZEKA, 2022

09 February 2023
Share

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema idadi ya watalii walioingia nchini katika kipindi cha Januari hadi Disemba 2022, imeongezeka hadi 1,454,920 ikilinganishwa na watalii 922,692 walioingia nchini katika kipindi hicho, mwaka 2021, ikiwa ni ongezeko la watalii 532,228 sawa na 57.7%, ambapo imebainisha kuwa ongezeko hilo limetokana na nchi nyingi kuondoa zuio la wananchi kusafiri nje ya nchi na filamu ya 'Tanzania the Royal Tour' iliyoongozwa na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.