Back to top

VITABU 16 VYAPIGWA MARUFUKU KUTUMIKA SHULENI.

13 February 2023
Share

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda, kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu 59 cha sheria ya Elimu, Sura 353 amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vya ziada kutumika katika shule za umma na binafsi nchini.

Prof. Mkenda ameyasema hayo jijini Dodoma ambapo amevitaja vitabu hivyo kuwa ni Diary of a Wimpy Kid, Diary of a Wimpy Kid -Rodrick Rules, Diary of Wimpy Kid - The Last Straw, Diary of Wimpy Kid-Dog Days, Diary of a Wimpy Kid The Ugly Truth, Diary of a Wimpy Kid -Cabin Fever, Diary of a Wimpy Kid - The Third Wheel na Diary of a Wimpy Kid - Hard Luck.

Vingine ni Diary of a Wimpy Kid - The Long Haul, Diary of a Wimpy Kid -Old School, Diary of a Wimpy Kid -Double Down, Diary of a Wimpy Kid-The Gateway, Diary, Diary of a Wimpy Kid-Diper Overlode, Is for TANSGENDER ( you know best who you are!), Is for LGBTQIA ( find the words that make you you) na Sex Education a Guide to life.

"Nahimiza wazazi mkague mabegi ya wanafunzi kuhakikisha vitabu hivi havitumiki nyumbani; ukaguzi na ufuatiliaji huu ni endelevu ili kubaini kama vitabu kama hivi hipo katika shule tuweze kichukua hatua,".Profesa Mkenda

Prof. Mkenda ametoa rai kwa watanzania kupiga namba 0262160270 ya mezani na 0737 962965 ya mkononi ili kutoa taarifa ya uwepo wa vitabu hivyo shuleni na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa shule yoyote itakayokutwa na vitabu hivyo ikiwemo kufutiwa usajili.