
Siku chache baada ya kutokea kwa vitendo vya uhalifu katika, Mtaa wa idara ya maji Bunju B, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema linawashikilia watuhumiwa sita halisi wa matukio hayo (Panya Road), pamoja na baadhi ya simu zilizoibiwa wakati wa uvamizi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salam, ACP Muliro Jumanne Muliro, amesema watuhumiwa hao baadhi yao wamekamatwa katika maeneo ya mapinga katika maeneo ya mabonde huku baadhi yao wakipatikana na baadhi ya vitu walivyoiba.
Muliro amebainisha hayo wakati wa operesheni iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika mitaa ya Bunju B, iliyohusisha Jeshi la Polisi na vikundi vya ulinzi shirikishi.
ACP Muliro amesema vitu walivyokamata ni pamoja pia na simu mbili ambazo zimetambuliwa na wamiliki wa simu hizo ambao ni miongoni mwa wakazi wa mtaa wa idara ya maji ambao kaya zao zilivamiwa.
