Back to top

WASIOJULIKANA WADHURU VIONGOZI MONDULI

18 February 2023
Share

Viongozi wa Kata ya Engaruka wilayani Monduli mkoani Arusha, waliokuwa wanafuatilia uharibifu wa vyanzo vya maji wavamiwa na kushambuliwa kwa silaha za jadi na watu wasiojulikana, tukio linalohusishwa na mgogoro mkubwa wa ardhi unaoendelea katika Kata hiyo.

Akizungumzia tukio hilo katika mkutano wa hadhara wa kushughulikia mgogoro huo, Mkuu wa Wilaya hiyo Bw.Suleimani Mwenda amesema kazi ya kuwatafuta na kuwakamata wote waliohusika katika tukio hilo inaendelea na amewataka wananchi kutoa ushirikiano.

Baadhi ya viongozi hao ambao baadhi yao wamejeruhiwa kwa mapanga, na mikuki wamesema udhaifu wa kusimamia sheria ni miongoni mwa sababu zinazochangia migogoro katika wilaya hiyo.

Kwa upande wao viongozi wa Halmashauri ya Monduli wamesema mgogoro katika Kata hiyo ni wa muda mrefu, na licha ya kuchukua baadhi ya hatua tatizo bado ni kubwa.

Engaruka ni miongoni mwa Kata za Wilaya ya Monduli, zinazokabiliwa na migogoro kwa muda mrefu inayohusishwa na kugombea ardhi ya malisho, kilimo na  matumizi mengine ambayo ambayo kwa sasa haitoshelezi mahitaji ya binadamu ,mifugo, na viumbe wengine wakiwemo wanyamapori,