Back to top

SERIKALI YAFIKIRIA KUZIFUTA SHULE 4 ZILIZODANGANYA

19 February 2023
Share

Serikali imesisitiza kuendelea kufanya uchunguzi na kuchukua hatua, ikiwezekana kuzifuta shule nne zilizofanya udanganyifu katika mitihani ya kidato cha nne mwaka 2022 na kusababisha Baraza la Mitihani Nchini, kuzuia na kufuta matokeo ya zaidi ya wanafunzi 300 waliokuwa wakisoma kwenye shule hizo.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Prof.Adolf Mkenda, wakati akizungumza na wazazi wa wanafunzi 140, waliokuwa wakisoma katika shule ya sekondari Thaqafa ambao matokeo yao yamezuiwa baada ya shule hiyo, kubainika kufanya udanganyifu.