
Naibu Waziri wa Afya, Dkt.Godwin Mollel amesema muafaka wa kuondokana na kero na malalamiko ya wananchi juu ya upatikanaji wa huduma ya Mfuko wa Afya Ngazi ya Jamii (CHF), ni kupitia muswada wa sheria ya bima ya afya kwa wote ambao utatoa nafasi kwa wananchi kupata huduma bora katika Hospitali zote nchini kuanzia Zahanati mpaka Hospitali ya Taifa.
.
Dkt. Mollel ameyasema hayo wakati akijibu risala ya Waganga Wakuu wa Mikoa (RMOs) na Halmashauri, katika mkutano wao uliofanyika, Jijini Dodoma, ambapo wamelalamikia ubovu wa Mfuko huo, kutokana na kutokukidhi mahitaji ya wananchi kupata huduma za afya katika maeneo mbalimbali nchini.
