
Jeshi la polisi mkoani Kagera, limesema tayari limemkamata kijana Paschal Kaigwa (22), ambaye anatuhumiwa kumbaka na kumuua mke wa Mwenyekiti wa Mtaa wa National Housing, uliopo Manispaa ya Bukoba, aitwaye Khadija Ismail mwenye umri wa miaka 29.
.
Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, William Mwampaghale amesema mtuhumiwa huyo alijificha katika vichaka na baada ya kukaa huko bila chakula, aliamua kutoka na kwenda nyumbani kwa shangazi yake, katika Mtaa wa Katatorwansi uliopo Manispaa ya Bukoba, ambapo aliwakuta watoto ambao baada ya kumuona walipiga kelele na kuwezesha wananchi kumkamata.
