Back to top

WALINDENI WATOTO, KATUNI ZINAZOHAMASISHA USHOGA

05 March 2023
Share

Jeshi la Polisi mkoani Geita limeitaka jamii kuchukua tahadhari kwa kuwalinda watoto dhidi ya filamu za katuni zenye maudhui yanayohamasisha na kuchochea mapenzi ya jinsia moja kwani zinachangia kuporomoka kwa maadili ya nchi pamoja na kuwaathiri watoto wadogo kisaikolojia.
.
Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Geita, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Bethaneema Mlay, wakati akitoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia kwa waumini wa kanisa la KKKT lilipo Nyankumbu mkoani humo.