
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, ACP Alex Mkama , amewataka madereva wa Bajaj na Pikipiki ambao hawana vyeti vya udereva kuhakikisha wanaenda kusoma udereva kwenye vyuo vinavyotambulika na serikali na kupata vyeti, kabla Jeshi hilo halijaanza operesheni ya kuwasaka ambao wataendesha vyombo hivyo bila kukidhi vigezo.
