Back to top

IDADI WALIOFARIKI AJALINI GEITA YAFIKIA 10

08 March 2023
Share

Vifo vilivyotokana na ajali ya basi la kampuni ya Sheraton, lililokuwa likitokea mkoani Mwanza kuelekea Ushirombo mkoani Geita, vimefikia 10 huku majeruhi 49 wakiendelewa kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita na Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando mkoani Mwanza.
.
Basi hilo lenye namba za usajili T 922 ADC lilitumbukia kwenye daraja lililopo Kasamwa nje kidogo ya Mji wa Geita, baada ya kupasuka gurudumu la mbele na kupoteza mwelekeo.