Back to top

WAZIRI MABULA ATAKA WANAWAKE KUJIAMINI

09 March 2023
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wanawake nchini kujiamini wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Amesema, wanawake wanatakiwa kufanya kazi zao huku wakielewa kuwa juu yao yupo mwanamke shujaa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.

Dkt.Mabula amesema wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Kwadeko wilayani Kwimba mkoani Mwanza.

“Kila mwanamke anayepewa nafasi akiwa mwenyekiti au kiongozi wa mahali fulani, anatakiwa kujiamini kwa kuwa wanawake wamemuweka pale"amesema Dkt Mabula.